Mlinzi wa zamani wa Barcelona Eric Abidal amejiunga tena na klabu yake ya zamani ya Monaco kwa mkataba wa miaka mitatu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 33 alirejea uwanjani mwezi April baada ya kupona maradhi ya Ini yaliyoa anza kumsumbua mwaka 2012.Hata hivyo baada ya kurejea klabu yake ya Barcelona ilimuacha huru mwishini mwa msimu baada ya kuitumikia kwa miaka sita Nou Camp.
Abidal, ambaye wakati mwingine hucheza nafasi ya ulinzi wa kati na ulinzi wa kushoto aliaanzia kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Monaco na baadaye kujiunga na Lille kisha ya nyumbani kwao ya Lyon.
Alishinda taji la ligi kuu ya Ufaransa akiwa na Lyon msimu wa 2007 kabla ya kujiunga na Barcelona kwa ada ya pauni milioni £10.Abidal aligundulika kuwa na tatizo la ini na kuelekea kufanyiwa upasuaji mwezi March mwaka 2011, lakini alirejea baada ya iezi iwili baadaye ambaye alishinda taji la Champions League baada ya Barca kuinyoa Manchester United katika mchezo wa fainali katika dimba la Wembley.
Mwezi April mwaka 2012 aliwekewa ini kutoka kwa ndugu yake.Monaco inayojengwa tena tayari imeshawasajili nyota wa kimataifa wa Ufaransa Jeremy Toulalan, mlinzi wa Real Madrid Ricardo Carvalho, nyota pacha wa Porto Joao Moutinho na James Rodriguez, mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao kutoka katika klabu ya Atletico Madrid.
No comments:
Post a Comment