Liverpool imepiga chini ombi la klabu ya Arsenal la kumtaka mshambuliaji wake Luis Suarez kwa ada ya pauni milioni.
Suarez amekuwa katikati ya tetesi za kuhama klabu hiyo tangu aliposema kuwa ana mpango wa kuhama mwezi wa Mei alipotumia maneno kuwa it would be a "good moment for a change", na kutumia maneno maengine kuwa "difficult to say no" kujiunga na Real Madrid.
Real Madrid ilikuwa ikitazamiwa kuelekeza ushawishi wao wa kumsawishi mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26-raia wa Uruguay.
Liverpool imekataa kuzungumza lolote juu ya taarifa ya Arsenal huku wakisisitiza kuwa Suarez is not for sale.
Chelsea pia walikuwa wakihusishwa na kumtaka Suarez na ilikuwa ikionekana kuwa Arsenal walikuwa vinara wa hilo ambapo meneja Arsene Wenger alikuwa akiendelea kumalizia mchakato kwanza wa Gonzalo Higuain wa Real Madrid.
Real wanatazamiwa kuathirika na kauli hiyo ya Liverpool ya kwamba Suarez hauzwi vinginevyo labda ni kwa ada ya pauni milioni £50 ambayo ilimng’oa Fernando Torres alipojiunga na Chelsea mwezi January 2011.
No comments:
Post a Comment