Manchester United imemtangaza Ryan Giggs kuwa kocha mchezaji huku Phil Neville akitarajiwa kutangazwa kuwa kocha wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo.Giggs ambaye anatarajiwa kufikia umri wa miaka 40 mwezi Novemba na mchezaji mwenzake wa zamani wa klabu hiyo Neville ambaye kwasasa ana umri wa miaka 36 ndio nyongeza mpya ya kocha mpya David Moyes katika safu ya watu wake wa pembeni katika benchi la ufundi Old Trafford.Amekaririwa Moyes akisema"Nimefurahi kwamba Ryan amekubali nafasi hiyo ya kuwa kocha mchezaji".Kwa upande wake Giggs ameongeza kwa kusema"Siyo siri nilikuwa nikichukua ujuzi wangu. Naliona hili kama ni hatua yangu ya mwanzo kwa hatma yangu ya baadaye katika soka"Ilitazamiwa kuwa klabu hiyo ingemtangaza Nevile mwenye umri wa miaka 36 kuwa kocha mpya wa kikosi cha kwanza kufuatia kuondoka klabu hapo kwa Rene Meulensteen.Giggs amendelea kwa kusema"Ni fahari kubwa kuajiriwa kama kocha mchezaji. Nina matumaini nitaweza kuleta ujuzi wangu karibu, nikifanya kazi kama mchezaji na sehemu ya familia ya Manchester United kwa kipindi kirefu."Naangalia mbele kufanya kazi sambamba na David na timu"Moyes ambaye alitajwa na mtangulizi wake Sir Alex Ferguson mwezi Mei, atafanya mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza hapo kesho Ijumaa kama meneja.Kiungo Giggs alisaini mkataba mwingine wa kuongeza msimu mwingine wa mwaka mmoja kama mchezaji ndani ya United mwezi machi, mkataba ambao utamuweka Old Trafford mpaka Juni 2014 ambapo atakuwa akikamilisha misimu 23 ya kuitumikia klabu hiyo
No comments:
Post a Comment