MCHEZAJI MPYA Neymar,
ataonekana kwa mara ya kwanza ndani ya Jezi ya Barcelona Uwanjani huko Poland
wakati Mabingwa hao wa Spain watakapocheza Mechi ya Kirafiki na Lechia Gdansk
Siku ya Jumatano.
Mechi hii ilikuwa
ichezwe mapema Mwezi huu lakini ilifutwa mara baada ya kutangazwa kuondoka kwa
Meneja wa Barcelona, Tito Vilanova, kwa matatizo ya maradhi ya
Kansa.
Kikosi ambacho
kitacheza huko Poland kina Vijana wengi lakini pia wapo Lionel Messi, Cristian
Tello na Alex Song na kitaongozwa na Kocha Msaidizi, Jordi Roura, huku Kocha
mpya Tata Gerardo Martino akibaki Barcelona na Wachezaji wengi wa Timu ya Kwanza
waliochelewa kurudi Mazoezini baada ya kuongezewa Likizo kwa vile walicheza
Kombe la Mabara huko Brazil Mwezi uliopita.
Neymar wakati anatambulishwa Barca siku za nyuma kidogo
No comments:
Post a Comment