Tottenham Hotspur ya England
imegoma kumuuza winga wake Gareth Bale kwenda Real Madrid pamoja na kupewa ya
uhamisho utakaoweza kuvunja rekodi ya dunia £82million. Inasemekana Spurs
kupitia mwenyekiti wake Daniel Levy wanataka walipwe kiasi hicho cha pesa pamoja
na wachezaji wawili wa Real Madrid Fabio Coentrao na Angel Di Maria ambao wote
kwa pamoja wana thamani ya £45m, hivyo kufanya thamani ya dili la Bale kwa jumla
kuwa £126 million ambazo ni fedha nyingi sana kuliko zile alizonunuliwa
Cristiano Ronaldo kutoka Manchester United £80m.
Bale anatarajiwa alipiwe £85m na Real Madrid kitu
ambacho kitakuwa ni Historia ya Dunia kwa Kwa kuuzwa kiasi hicho
kikubwa.Inasemekana pia Spurs wanataka kuongezewa wachezaji wawili tena pamoja
na dau hilo nono ambalo litaweka Historia.
Gareth Bale pia anatarajiwa kuongea na Klabu yake kuhusu uhamisho huo wa £85million kwenda kwenye Klabu ya Real Madrid
No comments:
Post a Comment