Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, July 9, 2013

AROUNA KONE ASAJILIWA NA EVERTON AKITOKEA WIGAN ATHLETIC


Everton imemsajili mshambuliaji wa Wigan Arouna Kone kwa mpango wa makataba wa miaka mitatu baada ya kuafiki kiasi cha pauni milioni £6 kilichotajwa na klabu yake.
Newcastle na Everton wote walifikia kiwango kwa ajili ya mshambulaiji huyo mwenye umri wa miaka 29 lakini mwenyewe Kone amechagua kuelekea Merseyside
Sasa atakutana na meneja Roberto Martinez, ambaye aliihama Wigan baada ya kumalizika kwa msimu uliopita.
Kone alifunga jumla ya mabao 11 ndani ya msimu uliopita katika ligi kuu ya England na michuano ya FA kabla ya kuteremka daraja na kuelekea Championship.
Bosi wa Wigan Owen Coyle alikaririwa wiki iliyopita akisema anatarajia Kone kuihama klabu hiyo na klabu anayokwenda ni Everton.
Martinez ambaye ameanza katika klabu ya Everton msimu uliopita alijiunga na Kone kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Levante ya Hispania kiangazi.
Kone aliwahi kuvichezea vilabu vya Belgiam Lierse SK, Udach Roda JC na PSV nchini Hispania ni katika klabu ya Sevilla.
Hata hivyo ada ya uhamisho haijawekwa wazi.

No comments:

Post a Comment