Pages

Monday, May 13, 2013

KIIZA AWEKA DAU MEZANI, ANAYEWEZA ASEME


Hamisi Kiiza na Haruna Niyonzima


MSHAMBULIAJI wa Kimataifa anayeichezea Yanga, Hamisi Kiiza ameweka mezani dau la Sh Milioni 50, ili aweze kusaini mkataba mpya.

Kiiza mkataba wake wa awali unatarajia kumalizika baada ya mechi yao dhidi ya Simba, itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mshambuliaji huyo aliyejiunga na Yanga katika msimu wa mwaka 2011/12 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ameonyesha nia ya kuendelea kuchezea timu hiyo, lakini akitoa masharti magumu kwa viongozi wake.
Habari zilizopatikana Dar es Salaam jana, kutoka ndani ya klabu hiyo, zilieleza kwamba mshambuliaji huyo, anahitaji kiasi hicho ili aweze kusaini mkataba huo.

Kilieleza kwamba, msimu huu hataki kusaini mkataba mpya kwa kulipwa kwa mapungufu kama alivyosajiliwa kwa mara ya kwanza akitokea URA ya Uganda.
Chanzo hicho kilisema endapo Yanga watakubali dau aliloweka mezani na Kiiza anataka alipwe fedha taslimu ili aweze kusaini.

Kilieleza hatakubali utaratibu uliotumika katika kipindi kilichopita ambaye alilipwa katika awamu mbili ya sehemu ya mkataba wake.
Wakati huo huo, imeelezwa Yanga ikishindwa kumpa fedha hizo, hatakuwa na sababu ya kuendelea kuichezea timu hiyo.

Kilieleza kwamba, pamoja na kuwepo kwa mazungumzo ya awali baina ya pande hizo mbili, lakini atakachoangalia ni maslahi binafsi.

No comments:

Post a Comment