Hamisi Kiiza na Haruna Niyonzima |
MSHAMBULIAJI wa Kimataifa anayeichezea Yanga, Hamisi Kiiza
ameweka mezani dau la Sh Milioni 50, ili aweze kusaini mkataba mpya.
Kiiza mkataba wake wa awali unatarajia kumalizika baada ya
mechi yao dhidi ya Simba, itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Mshambuliaji huyo aliyejiunga na Yanga katika msimu wa mwaka
2011/12 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ameonyesha nia ya kuendelea kuchezea timu
hiyo, lakini akitoa masharti magumu kwa viongozi wake.
Habari zilizopatikana Dar es Salaam jana, kutoka ndani ya
klabu hiyo, zilieleza kwamba mshambuliaji huyo, anahitaji kiasi hicho ili aweze
kusaini mkataba huo.
Kilieleza kwamba, msimu huu hataki kusaini mkataba mpya kwa
kulipwa kwa mapungufu kama alivyosajiliwa kwa mara ya kwanza akitokea URA ya
Uganda.
Chanzo hicho kilisema endapo Yanga watakubali dau aliloweka
mezani na Kiiza anataka alipwe fedha taslimu ili aweze kusaini.
Kilieleza hatakubali utaratibu uliotumika katika kipindi
kilichopita ambaye alilipwa katika awamu mbili ya sehemu ya mkataba wake.
Wakati huo huo, imeelezwa Yanga ikishindwa kumpa fedha hizo,
hatakuwa na sababu ya kuendelea kuichezea timu hiyo.
Kilieleza kwamba, pamoja na kuwepo kwa mazungumzo ya awali
baina ya pande hizo mbili, lakini atakachoangalia ni maslahi binafsi.
No comments:
Post a Comment