KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC na timu ya Taifa ‘Taifa
Stars’ Abubakari Salum ‘SureBoy’ amekataa ofa ya mshahara Sh milioni mbili
iliyotolewa na Yanga ili waweze kupata saini yake.
Yanga ambao wanahitaji saini ya kiungo huyo, walikuwa tayari
kumpa Sh milioni 50, ikiwa ni dau la usajili wake wa msimu ujao wa Ligi Kuu
Tanzania Bara.
Mabingwa hao wa ligi hiyo, ambao walikuwa na nia ya
kumchukua kiungo huyo, wanaweza kumkosa baada ya kumahidi kulipwa mshahara wa
Sh milioni mbili anaolipwa na klabu yake ya Azam FC.
Habari zilizopatikana
Dar es Salaam jana, kutoka ndani ya klabu hiyo, zilieleza kwamba kiungo huyo
ameshindwa kushawishika na fedha ambazo walipanga kumpa.
Chanzo hicho kilieleza kwamba kiungo huyo, anaona kiasi
alichotengewa ni kidogo kwani fedha hizo ndizo anazolipwa katika klabu yake ya
Azam.
Kilieleza kwamba, Yanga wangepandisha dau angeweza kukubali
kuondoka Azam FC kutokana na mkataba wake unatarajia kumalizika Desemba mwaka
huu.
“Yanga ilikuwa inamhitaji Sureboy lakini amekataa kutokana
na kutoshawishika na kiasi alichotajiwa,” kilieleza chanzo chetu.
Chanzo hicho kilieleza kwamba, sababu nyingine iliyomfanya
akatae kujiunga na Yanga ni baada ya Kocha Mkuu wa Azam FC, kumhakikishia kuwa
atamwongezea mkataba mpya.
Kilieleza kwamba, kiungo huyo, ameona ni bora abaki Azam FC,
ambaye ameahidiwa kulipwa donge nono baada ya mkataba wake wa awali kumalizika
kuliko kwenda Yanga kwa dau la Sh Milioni 50.
No comments:
Post a Comment