Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya
Tanzania (Taifa Stars) akimaliza mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon za
kilomita 21 zilizofanyika mjini Moshi.
Meneja wa Bia ya Kiliamanjaro, Geogre Kavishe
akimpongeza Edina Joseph mmoja wa washiriki wa mashindano ya
Kilimanjaro Marathon, yaliofanyika Moshi Mkoa wa Kilimanjaro, mashindano hayo
yalidhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, Premium Lager, Gapco, Vodacom , Tanga
Cement , CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, Tanzania one, New
ArushaHotel, UNFPA, Fastjet, Cluods FM, na Kilimanjaro Water. Picha: Executive
Solutions
Na Mwandishi
Wetu,Moshi
MWANARIADHA wa Kitanzania, Sarah
Ramadhani, jana aliibuka shujaa katika mashindano ya mwaka huu ya mbio ndefu za
Kilimanjaro Premium Lager Marathon, baada ya kuibuka mshindi katika mashindano
ya kilomita 21, (nusu marathon), kwa upande wa wanawake katika mbio
zilizofanyika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Sarah alishinda
mbio hizo baada ya kukimbia kwa dakika 1:13:05 na kujipatia medali ya dhahabu
baada ya kuwabwaga wenzake wakiwemo Wakenya ambao wamekuwa wakitawala mbio hizo
katika miaka ya hivi karibuni.
Katika mbio hizo
ambazo mwaka huu zimeweka rekodi ya kuwa na washiriki zaidi ya 6,800, Vicoty
Chepkemoi, kutoka Kenya alishika nafasi ya pili baada ya kukimbia kwa dakika
1:14:34, ambapo Mtanzania mwingine Failuna Matanga, alishika nafasi ya tatu kwa
kukimbia kwa dakika 1:15:35.
Hata hivyo wakenya waliendeleza
ubabe wao, baada ya wanariadha wake kushika nafasi ya kwanza katika mbio za
kilomita 42 na kilomita 21 wanaume, pamoja na nafasi ya kwanza katika kilomita
42 upande wa wanawake.
Katika mbio za kilomita 42
wanaume, Kipsang Kipkemoi alishika nafasi ya kwanza kwa kukimbia dakika 2:14:56
na kufuatiwa na mkenya mwenzake Julius Kilimo, aliekimbia kwa dakika kwa dakika
2:15:44 ambapo mkenya mwingine Dominic Kiangor alishika nafasi ya tatu kwa
kukimbia dakika 2:16:25.
Kwa upande wa wanawake, mkenya
Edna Joseph, alishinda mbio hizo pale alipomaliza kwa dakika 2:39:05 na
kufuatiwa na Eunice Muchiri, (Kenya), aliekimbia kwa dakika 2:41:00 na watatu
alikuwa ni Fridar Too, aliekimbia kwa dakika 2:44:04.
Akiongea muda mfupi baada ya
kuwazawadia washindi, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela
Mukangara, aliahidi ushirikiano wa serikali katika kuendeleza michezo hapa
nchini.
“Nichukue nafasi
hii kuwapongeza wadhamini wa mbio hizi, Kilimanjaro Premium Lager pamoja na
wadhamini shirikishi mbalimbali wa mashindano haya wakiongozwa na mdhamini mkuu,
kwani mbali na kuibua na kukuza vipaji vipya, mashindano haya yametokea kuwa
mchango mkubwa katika kuitangaza Tanzania na kukuza uchumi wa Kilimanjaro na
nchi kwa ujumla kutokana na kushirikisha watu wengi kutoka ndani na nje ya
nchi”, alisema.
Aliwataja wadhamini wengine
kuwa ni pamoja na Vodacom Tanzania, GAPCO, Tanga Cement, CFAO Motors, KK
Security, Keys Hotel, TPC Sugar, Tanzanite One, New Arusha Hotel, UNFPA, Fastjet
na Kilimanjaro Water.
Aidha alitoa changamoto kubwa
kwa viongozi wa riadha nchini kuhakikisha wanariadha wa Tanzania wanaandaliwa
vyema na mapema ili kuendeleza ushindi, ambapo alisema ushindi wa Sarah na
Failuna Makanga na mfano mzuri wa matayarisho mema.
Kwa upande wake Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema kuwa
mbio hizi zimeweza kuleta hamasa kwa watu mbalimbali kushiriki mchezo wa riadha
kwani Kilimanjaro Marathon ni tukio pekee la kimichezo ambalo linatoa fursa kwa
watu wote kushiriki. “Tutaendelea kuwekeza katika riadha kwa kadri tuwezavyo kwa
sababu Kilimanjaro Marathon sio tu kwa sababu imeishakuwa tukio linalosubiriwa
na wanariadha wetu kila mwaka lakini pia ni tukio ambalo limeendelea kuitangaza
nchi yetu kimataifa”, alisema.
Kavishe alisema tangu mbio hizi
zilipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2003, Kilimanjaro Premium Lager iliamua
kudhamini tukio hili kwa kuzingatia umuhimu wake kwa nchi yetu katika kukuza na
kuendeleza mchezo wa riadha na vilevile kuutangaza Mlima Kilimanjaro ambao ni
fahari ya Watanzania kama ilivyo bia yao ya Kilimanjaro Premium
Lager.
Meneja wa Bia ya Kiliamanjaro,
Geogre Kavishe akimpongeza Edina Joseph mmoja wa washiriki wa
Mashindano ya Kilimanjaro Marathon, yaliofanyika jana, Moshi Mkoa wa
Kilimanjaro, mashindano hayo yalidhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, Premium Lager,
Gapco, Vodacom , Tanga Cement , CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar,
Tanzania one, New ArushaHotel, UNFPA, Fastjet, Cluods FM, na Kilimanjaro Water.
(Picha: Executive Solutions)
2. Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya
Tanzania Taifa Stars akimaliza mbio ya Kilimanjaro Premium Lager Marathon za
kilomita 21 zilizofanyika jana mjini Moshi. (Picha: Executive Solutions
No comments:
Post a Comment