Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 27, 2013

YANGA YAZIDI KUJIIMARISHA KILELENI, YAIFUNGA KAGERA SUGAR 1-0 UWANJA WA TAIFA

Beki wa Yanga Mbwiyi Twite akipangusa kiatu cha Haruna Niyonzima baada ya kufunga bao


                                                         Jeeryson Tegete akiwatoka mabeki wa Kagera Sugar

                    Wachezaji wa Yanga wakitoka uwanja baada ya mchezo kumalizika

 
TIMU ya Yanga leo imeifunga Kagera Sugar bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa uwanja wa Taifa.
Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe pointi 42, baada ya kucheza mechi 18, hivyo kuwa kileleni mwa Ligi Kuu, ikiizidi Azam FC kwa pointi sita, ambayo inashika nafasi ya pili kwa pointi zake 36, huku mabingwa watetezi, Simba SC wanashika nafasi ya tatu kwa pointi zao 31.

Kagera inabaki na pointi zake 28 katika nafasi ya tano, baada ya kucheza mechi 19, chini ya Coastal Union ya Tanga inayoshika nafasi ya nne kwa pointi zake 30.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Simon Mberwa kutoka Pwani, aliyesaidiwa na Milambo Tshikungu wa Mbeya na Saada Tibabimale kutoka Mwanza, hadi mapumziko, hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake
 
Bao la Yanga lilifungwa na Haruna Niyonzima kipindi cha pili dakika ya 65 baada ya kupokea Oscar Joshua.
 
Kipindi cha kwanza dakika ya 45 Didier Kavumbangu alikosa penalti baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa faulo na mlinda mlango wa Kagera Sugar, Hannington Kalyesubula
 
Kwenye uwanja wa Manungu wenyeji Mtibwa watoshana nguvu na Prison ya Mbeya kwa suluhu ya 0-0.
 
 

No comments:

Post a Comment