TIMU ya New
Habari FC inatarajia kuanza mazoezi rasmi kesho kwa ajili ya kuajiandaa na
Mashindano yanayoandaliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
itakayoanza Machi 9 kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa
New Habari FC, Mohamed Mharizo, amesema mazoezi hayo yatafanyika kwenye uwanja
wa Shule ya Mugabe kuanzia saa kumi alasiri.
“Tunaanza
mazoezi Jumatano kwa ajili ya mashindano ya NSSF Cup, hivyo wachezaji wote
wanatakiwa kufika uwanjani bila kukosa,” alisema Mharizo.
Alisema
kabla ya kuanza kwa mashindano hayo, watacheza mechi moja ya kirafiki, kwa
ajili ya kuajiandaa na mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment