Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, January 7, 2013

YANGA KWENYE KIBARUA KINGINE KESHO

Timu ya Young Africans Sports  Club kesho itashuka dimbani kucheza na timu ya Denizlispor FC ya ligi daraja la kwanza nchini Uturuki katika mchezo wa kirafiki            utakaofanyika katika uwanja wa Selen Football -Kalimya Complex pembeni kidogo ya mji wa Antlaya.

Young Africans ambayo imeweka kambi ya mafunzo jijini Antalya itatumia mchezo huo kama fursa ya kujipima nguvu na timu hiyo la Denizlispor FC  ambayo imeshuka kutoka ligi kuu ya Uturuki mwaka jana na sasa inapamabana kurudi tena katika Ligi Kuu ya Uturuki.
Kocha Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kupata nafasi ya kucheza na timu kubwa kama ya Denizlispor FC ambayo ina wachezaji wa kiwango cha kimataifa hivyo anaamini utakua ni mchezo safi na kuwavutia.


Baada ya kuwa na wiki moja ya mazoezi na mechi moja ya kirafiki dhidi ya Armini Bielefeld ya ujerumani mwishoni mwa wiki itakua ni fursa nyingine nzuri ya kucheza mchezo wa kirafiki na timu nyingine, hii itanisadia kuona maendeleo ya kikosi changu kutokana na mazoezi ambayo tumekuwa tukiyafanya tangu tulipofika alisema 'Brandts'
Denizlispor FC ni miongoni mwa timu zaidi ya 200 kutoka shemu tofauti duniani ambazo zimeweka kambi katika mji wa Antlaya kwa ajili ya maandilizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la kwanza nchini Uturuki.
Mchezaji wa zamani wa Leicester City ya Uingereza, Dundee United ya Scotland na Ivernes ya Uholanzi, Mtanzania mzaliwa wa Uingereza Eric Odhiambo ni miongoni mwa washambuliaji wa kutegemewa wa timu ya Denizlispor FC. 
Young Africans imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne tayari kabisa kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa kesho katika uwanja wa Selen Football - Kalimya complex pemebeni kidogo ya mji wa Antalya. 

Kikosi cha wachezaji 27 waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na hakuna majeruhi hata mmoja hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia mchezaji yoyote katika mchezo huo. 

Athumani Idd 'Chuji' na Hamis Kiiza waliokuwa wakijisikia vibaya kabla ya mchezo wa juzi dhidi ya Amrnini Bielefeld wanaendelea vizuri kabisa kwani wanaendelea na mazoezi pamoja na wachezaji wengine waliopo na timu mjini Antalya.  

Kuhusu hali ya hewa leo haijaonekana kuwa tatizo kwa wachezaji kwani wanaonekana kuimudu na muda mwingi kwa kuwa jua linalowaka kuanzia asubuhi wakati wa mazoezi mpaka jioni, kwa leo hali ya hewa ni nyuzi joto 17 - 21, hivyo hali ya hewa ni nzuri.

No comments:

Post a Comment