Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, October 23, 2012

MTIBWA SUGAR, JKT RUVU SASA KUCHEZA NOV 7

SHIRIKISHO la Soka nchini Tanzania limepangua tena ratiba ya ligi kuu ambapo mechi namba 79 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Mtibwa Sugar na JKT Ruvu iliyopangwa kuchezwa Novemba 3 mwaka huu Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro, sasa itafanyika Novemba 7 mwaka huu.
 
Mabadiliko hayo yamefanyika kwa vile Novemba 4 mwaka huu, Mtibwa Sugar itacheza mechi namba 30 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro. Mechi hiyo awali ilikuwa ichezwe Oktoba 3 mwaka huu lakini ikabadilishwa ili kutoa fursa kwa mechi za Super Week zilizooneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Super Sport cha Afrika Kusini.
 

No comments:

Post a Comment