Na Rahel Pallangyo
SHIRIKISHO
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema watalinda haki walizouzia Benki ya
Taifa ya Biashara (NBC) kwa mujibu wa mkataba waliosaini.
Kauli hiyo
ilitolewa na Mkurugenzi wa Sheria, Habari na Masoko wa TFF, Boniface Wambura,
Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa nembo rasmi ya ligi ya Championship
ambayo mdhamini wake ni NBC.
"TFF
tuna furaha kupata mdhamini mmoja kwenye bidhaa zetu tatu kwa wakati mmoja
hivyo nawahakikishia NBC kuwa haki tulizowauzia tutazilinda kwa mujibu wa
mikataba tuliyosaini,” alisema Wambura.
Naye
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Elibariki Masuke alisema katika mkataba
waliosaini Agosti 11 na TFF kipengele cha tatu kinazungumzia udhamini wa ligi
ya Championship.
“Leo hii
tuko hapa kutimiza sehemu ya jukumu letu la kimkataba na udhamini kuzindua
chapa mpya ya Ligi ya Daraja la Kwanza (Championship) na kuipa jina la NBC
Championship League kama sehemu ya uzinduzi wa mashindano haya ya soka
yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni,” alisema.
Agosti 11,
mwaka huu jijini Tanga, NBC ilitangaza kuingia makubaliano ya kuongeza
muda wa kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kipindi cha miaka mitano mingine
kuanzia msimu wa mwaka 2023/24 hadi mwaka 2027/2028 na kuongeza Ligi ya
Championship na First League.
Mkataba wa awali wa udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara wa miaka
mitatu ulikuwa wa thamani ya Sh bilioni tisa ambapo utamalizika msimu ujao wa
mwaka 2023/2024 na sasa wameingia makubaliano mapya ya mkataba wenye thamani ya
Sh bilioni 32.56.
Wakati wakisaini makubaliano hayo NBC kupitia Mkurugenzi
Mtendaji, Theobald Sabi, alisema
Ligi ya Championship na First league zote zitapewa majina ya
benki hiyo baada ya utaratibu kukamilika.
NBC Championship League inashirikisha timu 16 na inatarajiwa
kuanza kesho kwa kuchezwa michezo mitano katika viwanja vya miji tofauti na
mingine mitatu itachezwa keshokutwa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment