CBE QUEENS |
JKT QUEENS |
Na Rahel Pallangyo
JKT Queens imetinga fainali ya Ligi ya Mabingwa
Afrika kwa wanawake kwa ukanda wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na
Kati (CECAFA) kwa kuifunga Buja Queens ya Burundi kwa mabao 3-1 Uwanja wa FTC
Njeru, Kampala leo
Kwa ushindi huo JKT Queens itacheza fainali na CBE ya Ethiopia ambayo iliifunga Vihiga Queens ya Kenya kwa mabao 2-1, Jumatano ijayo Agosti 30, 2023.
Katika mchezo huo wa nusu fainali ulioanza saa 6:00
mchana JKT Queens walikwenda mapumziko wa kiwa nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa
na Teopistar Situma dakika ya 11.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku JKT
wakionekana kubadilika kwani waliliandama lango la Buja Queens na dakika ya 61
Donisia Minja alifungua kitabu cha mabao akimalizia mpira uliopanguliwa na kipa
wa Buja uliotokana na shuti la Stumai Abdallah.
Katika
kuonesha kuwa JKT Queens wanahitaji kufuzu fainali dakika ya 77, kiungo
mfupi mwenye makeke uwanjani Stumai
Abdallah alifunga bao la pili akimalizia mpira wa krosi iliyopigwa na Amina
Bilal na kuibua shangwe kwa mashabiki na benchi la ufundi.
Wanasema haiwezi kuisha bila kumalizika kabisa kwani
JKT Queens ambao walikuwa na uchu wa mabao zaidi, mshambuliaji kinda Winifrida
Gerald alifunga bao la tatu kwenye dakika za nyongeza akimalizia mpira wa
adhabu uliopigwa na Anastazia Katunzi baada ya Stumai kufanyiwa madhambi.
JKT Queens katika makundu waliifunga AS Kigali ya
Rwanda mabao 2-1 kabla ya kuibamiza New Generation ya Zanzibar bao 1-0 kisha
kuikandamiza Vihiga Queens ya Kenya bao 1-0.
Mwisho
No comments:
Post a Comment