Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, April 16, 2018

SIMBA YAIFUNGA PRISONS 2-0 TAIFA, ALHAMISI KUCHEZA NA LIPULI
JOHN Bocco na Emmanuel Okwi leo wameipatia Simba ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Prisons katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Ushindi huo unaifanya Simba izidi kujisafishia njia kuelekea kwenye ubingwa kwani sasa inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 58 juu ya mabingwa watetezi Yanga walio na pointi 47 na mechi mbili kibindoni.
Mabao ya Simba yalifungwa katika kila kipindi kwenye mechi hiyo hiyo ambayo vinara hao walitawala katika vipindi vyote.
Prisons ilionekana kuibana Simba katika dakika za mwanzo kabla ya kusalimu amri na kuruhusu bao la Bocco dakika ya 35 kabla ya kujikuta wakicheza mchezo wa kujilinda zaidi katika kipindi cha pili.
Bocco alifunga bao hilo la kuongoza kwa kuuwahi kwa kichwa mpira wa krosi wa Erasto Nyoni uliogonga mwamba kabla ya kuujaza wavuni.
Okwi aliifungia Simba bao la pili katika dakika ya 80 na kuendelea kukifukuzia kiatu cha dhahabu kwa kufikisha mabao 18 kwenye ligi.
Penalti ya Okwi ilitolewa na mwamuzi Shomari Lawi wa Kigoma baada ya Jumanne Elifadhili kumfanyia madhambi Bocco akiwa kwenye eneo la hatari, Elifadhili alioneshwa kadi nyekundu.
Katika mechi hiyo Simba ilikosa mabao mengi hasa kupitia kwa mchezaji wake Shizza Kichuya aliyekosa mabao dakika ya kwanza, 50, 62 na 70.
Mechi nyingine zilizochezwa Ndanda ikiwa nyumbani Nang'wanda Sijaona imeshindwa kutamba kwa kukubali ‘kupapaswa’ na Ruvu Shootinga mabao 3-1 huku Kagera Sugar ikishinda 2-1 dhidi ya ndugu zake Mtibwa Sugar kwenye uwanja wake wa nyumbani Kaitaba.