Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, April 16, 2018

MAGUFULI, MONALISA NA RAY WAPATA TUZO ZA APA GHANA


RAIS Magufuli na waigizaji wa filamu  Yvonne Cherrie 'Monalisa' na Ray Kigosi wameibuka washindi kwenye tuzo za kifahari za Afrika 'The African Prestigious Awards' nchini Ghana
Katika tuzo hizo zilizotolewa juzi Accra nchini Ghana, Monalisa ametwaa tuzo katika kipengele cha mwigizaji bora barani Afrika na kumbwaga mpinzani wake Lupita Nyong'o.
Ray Kigosi ameshinda tuzo ya mwigizaji bora wa kiume barani Afrika na Moiz Hussein alishinda katika kipengele cha mpigapicha bora
Monalisa alithibitisha ushindi huo kupitia mtandao wake wa Instagram akiwa na picha ya tuzo yake na kuandika, “Tumeshindaaaaaaa narudi nyumbani na tuzo za kutosha, ahsante Watanzania, nawapenda mno,”.
Kwa ujumbe huo wa Monalisa ina maana huenda pia kuna tuzo nyingine Watanzania ambazo wameshinda kwani  walikuwa wanawania vipengele mbalimbali katika tuzo.
Watanzania wengine waliokuwa wanawania ni King Majuto kipengele cha mchekeshaji bora Afrika, Vicent Kigosi kipengele cha msanii bora wa kiume Afrika na mpigapicha mahiri ambapo alikuwepo Moiz Hussein
Monalisa kabla ya kuondoka alikatiwa tiketi ya ndege na kuagwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.