Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, March 21, 2018

YANGA KUANZA NYUMBANI KOMBE LA SHIRIKISHO CAF KUCHEZA NA DICHA YA ETHIOPIA



YANGA imepangwa kucheza na Welayta Dicha ya Ethiopia katika mechi ya mchujo ya michuano ya Kombe la Shirikisho.
Kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa makao makuu ya Shirikisho la soka Afrika (CAF), Cairo Misri leo Yanga itakuwa mwenyeji wa mechi ya kwanza mapema mwezi ujao kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Kufikia hatua hiyo, Dicha iliitoa Zamalek ya Misri baada ya kila mmoja kushinda mabao 2-1 kwao kabla ya kuwatoa mabingwa hao wa zamani wa Afrika kwa matuta.
Kabla ya kucheza na Zamalek, ilicheza na Zimamoto ya Zanzibar na kutoka nayo sare ya bao 1-1 katika mechi ya kwanza Zanzibar kabla ya kushinda bao 1-0 nyumbani Ethiopia.
Dicha inaonekana ni timu dhaifu kwani inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Ethiopia inayoshirikisha timu 16 ikiwa na pointi 19 katika mechi 15 ilizocheza.
Yanga imeangukia kwenye michuano hiyo baada ya kutupwa nje kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 2-1 iliyofungwa nyumbani uwanja wa Taifa na Township Rollers ya Botswana kabla ya kwenda kulazimisha suluhu ugenini Gaborone.
Mwaka juzi Yanga pia ilishiriki michuano hii baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa na Al Ahly ambapo ilicheza na Esperanca ya Angola kwenye kombe la Shirikisho na kufuzu hatua ya makundi.

No comments:

Post a Comment