Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, March 21, 2018

NGORONGORO HEROES RAHA SANA, YAIADHIBU MSUMBIJI 2-1





TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes leo imeshinda mabao 2-1 dhidi ya wenzao wa Msumbiji katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Huo ni ushindi wa pili kwa Ngorongoro katika mechi za kirafiki za kimataifa baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita kuifunga Morocco bao 1-0.
Katika mechi hiyo, wageni Msumbiji walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 13 likiwekwa kimiani na Martinho Alberto kwa mkwaju wa penalti baada ya kipa wa Ngorongoro Aboutnalib Mshery kumchezea vibaya mchezaji wa Msumbiji aliyekuwa akielekea kufunga.
Mshambuliaji Abdul Suleiman aliisawazishia Ngorongoro bao baada ya kuunganisha pasi ya Said Bakari akiwa ndani ya 18 na kwenda mapumziko wakiwa sare ya bao 1-1.
Dakika ya 59 nusura Ngorongoro ipate bao la mkwaju wa penalti iliyotolewa na mwamuzi baada ya mchezaji wake kuchezewa vibaya na wa Msumbiji, lakini Hasad Juma aliyepewa dhamana ya kupiga penalti hiyo alikosa.
Bao la pili la vijana hao wa kocha Amy Ninje lilifungwa dakika ya 69 na Said Bakari kwa shuti kali ndani ya 18.
Baada ya mechi hizo, Ngorongoro sasa inajiandaa na mechi ya kuwania kufuzu michuano ya Afrika kwa vijana wa umri huo dhidi ya Congo DR mwishoni mwa mwezi huu kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment