Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, March 14, 2018

WAMBURA AFIKISHWA KAMATI YA MAADILI KUJIBU TUHUMA TATU ZINAZOMKABILI


Image result for WAMBURA
SHIRIKISHO la Soka limempeleka kwenye kamati ya Maadili leo Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura kwa makosa matatu ya kupokea fedha za TFF malipo yasiyo halali, kugushi  barua na kushusha hadhi ya TFF.
Akizungmza leo Kaimu Ofisa habari, Cliford Ndimbo alisema Wambura amefikishwa kwenye kamati ya Maadili na Sekretarieti ya TFF baada ya Kamati ya Ukaguzi kukutana na kupitia mambo mbalimbali ya ukaguzi na suala hilo la Wambura kuonekana anatakiwa kufika kwenye Kamati ya Maadili.
Kamati ya Maadili imepokea malalamiko yanayomhusu Wambura ikiwa ni uvunjifu wa kanuni za Maadili Tolea la 2013 na Katiba ya TFF kama ilivyorekebishwa mwaka 2015.
Wito huo umemtaka Wambura kufika mbele ya Kamati ya Maadili leo na ana hiari ya kufika kutoa utetezi huo kwa njia ya mdomo, kutuma kwa maandishi, kuleta mashahidi au kutuma mwakilishi akiambatana na barua ya uwakilishi.
Makosa anayoshtakiwa Wambura ni; 1.Kupokea/Kuchukuwa fedha za Shirikisho (TFF) za malipo ambayo hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013
2. Kughushi barua ya kueleza alipwe malipo ya Kampuni ya JECKS SYSTEM LIMITED huku akijua malipo hayo sio halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013
3. Kufanya Vitendo vinavyoshusha hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume na Ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF (Kama ilivyorekebishwa 2015)