Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, March 5, 2018

WAAMUZI WANNE WA TANZANIA WACHUNGUZWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA NA CAF


Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Kidao Wilfred (katikati) akitoa ufafanuzi kuhusu waamuzi wa kimataifa wa Tanzania wanaotuhumiwa kwa rushwa katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika kati ya Lydia ya Burundi na Rayon ya Rwanda. Kushoto ni Katibu Mkuu wa DRFA, Msanifu Kondo na Kaimu Ofisa habari wa TFF, Clinford Ndimbo. (Picha na Rahel Pallangyo)


WAAMUZI wa Soka wanne wa Kimataifa wa Tanzania wanatuhumiwa kwa rushwa na Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) suala hilo limepelekwa kamati ya nidhamu ya CAF.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Kidao Wilfred alisema walipata barua  Februari 23 kutoka CAF kuwa mchezo wa mabingwa Afrika dhidi ya Rayon (Rwanda) na Lydia (Burundi) ulikuwa na matatizo.
“Tuliambiwa tujieleze kwa sababu waamuzi waliokwenda kuchezesha Mfaume Nassoro, Frank Komba, Soud Lila na Israel Mujuni walitoka Tanzania,”
“Siku moja kabla ya mchezo kulitokea na sintofahamu kwenye hoteli waliyofikia waamuzi na  inasadikika viongozi wa Rayon walikutwa kwenye chumba cha mmoja wa waamuzi wetu lakini siku hiyo hiyo kulitokea fujo baina ya viongozi wa timu mgeni (Rayon) na viongozi wa Lydia ikalazimika polisi kuingilia kati,” alisema Kidao.
Baada ya matukio hayo polisi iliwashikilia viongozi wa timu mgeni na kamishna wa mchezo huo ambaye ni Gradmoo Mzambi kutoka Zimbabwe alitoka baada ya kusikia kelele na ikaitaarifu CAF kuhusu kilichotokea.
Kidao alisema Februari 27 waliaindikiwa tena barua na CAF kutaka maelezo ya tukio hilo yawe yamewafikia kabla ya Machi 6 na wao ilibidi kufanya uchunguzi kabla ya kuiandikia CAF.
Anasema taarifa ya kamishna wa mchezo huo ndio inaweza ikawasafisha au kuwahukumu kwa sababu kwenye hoteli waliyofikia kulikuwa na CCTV kamera na imeambatanishwa kwenye ripoti ya kamishna.
“Jambo hili limepelekwa kwenye kamati ya nidhamu ya CAF na bdio italitolea maamuzi lakini sekretarieti ya TFF itakutana na kamati ya waamuzi ya Tanzania kujadiliana lakini hatuwezi kutoa maamuzi hadi CAF walifanyie kazi,” alisema Kidao
Kidao anasema TFF inataka haki itendeke hata kama waamuzi wetu watakuwa wamefanya makosa kwani ni jambo ambalo halina twasira nzuri kwa maendeleo ya soka.
Katika mchezo huo wa klabu bingwa barani Afrika Rayon ilifunga Lydia 1-0 na kufanikiwa kusonga mbele.

No comments:

Post a Comment