Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, March 5, 2018

IRINGA FC MABINGWA WA LIGI DARAJA LA TATU

Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava (kushoto) akiwa na mgeni rasmi Fesail Asas wakimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Iringa United baada ya kuwafunga Mtwivila City kwa penalti baada ya kumaliza dakika tisini wakiwa wamefungana bao 1-1 
 
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi zawadi ya jezi kampteni wa timu ya Mtwivila baada ya kuwafungwa na timu ya Iringa United kwa njia ya mikwaju ya penalti baada ya kumaliza dakika tisini wakiwa wamefungana bao 1-1

Mashabiki na viongozi wa timu ya Iringa United wakishangilia ushindi baada ya kuwafunga timu ngumu ya Mtwivila City kwa njia ya mikuju ya penati na kuwa wawakilishi wa mkoa wa Iringa kwenye ligi ya mabingwa wa mikoa


TIMU ya Soka ya Iringa United imetwaa ubingwa wa ligi ya daraja la tatu Mkoa wa Iringa baada ya kuibuka na ushindi penalti 3-1 dhidi ya Mtwivila FC.
Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Samora  juzi timu ya Mtwivila FC walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya nane lililofungwa na mshambuliaji David Mwanga kwa uzembe wa golikipa wa Iringa United Nelly Mkakilwa kumpita tobo.
Mchezo huo uliokuwa wa kukamiana lakini baadhi ya wachezaji wakionyesha ufundi katika kucheza mpira, hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Mtwivila walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, kila timu ikionyesha haijabahatisha kufika fainali huku Mtwivila wakitaka kuongeza na Iringa wakitaka kusawazisha.
Mchezaji wa Iringa, Razack Kibuga aliibuka shujaa baada ya kusawazisha bao katika dakika ya 76 na kuwaacha wachezaji wa Mtwivila wakilaumiana baada ya dakika 90 kumalizika ndipo wakapigiana penalti na Iringa ikashinda penalti 3-1 za Mtwivila  
Kutokana na ushindi huo timu ya Iringa United ilijinyakulia kikombe, jezi seti moja na mipira miwili na timu ya Mtwivila waliondoka na jezi na mpira mmoja.
Mchezaji bora ni Razack Kibuga wa Iringa United aliondoka na zawadi ya sh.100,000 na cheti golikipa bora alikuwa Nelly Mkakilwa toka Iringa United aliyepata sh.50,000

Nafasi ya tatu ilichukuliwa na timu ya Mkimbizi FC baada ya kuifunga timu ya Mshindo FC kwa mabao 5-4.

No comments:

Post a Comment