Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, February 9, 2018

TENGA: MWENYEKITI MPYA WA BMT

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kwa mujibu wa Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ya mwaka 1967 pamoja na marekebisho yake  ikisomwa na muundo wa shughuli za Baraza, amemteua Leodger Chilla Tenga kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa.

Dk. Mwakyembe amewateua pia wajumbe wapya sita wa Baraza hilo  kama ifuatavyo:

1.    Profesa Mkumbwa M. A. Mtambo.
2.    Beatrice Singano.
3.   Kanali Mstaafu Juma Ikangaa.
4.   John Joseph Ndumbaro.
5.   Rehema Sefu Madenge.
6.    Salmin Kaniki.

Aidha, Dk. Mwakyembe amewateua wajumbe wengine watatu wa Baraza kutokana na nafasi za vyeo vyao ambao ni:

1.    Yussuph Singo - Mkurungezi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo.
2.   Dk. Edicome Shirima- Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia  na Mafunzo ya Ufundi.
3.   Mohammed Kiganja-Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa ambaye atakuwa ni Katibu wa Baraza.
Uteuzi wa wajumbe wote umeanza rasmi Februari 8, 2018 na watalitumikia Baraza kwa kipindi cha miaka mitatu


Vilevile Dk. Mwakyembe kwa mujibu wa sheria amemteua Timothy Mganga kuwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kwa kipindi cha miaka mitano.  

No comments:

Post a Comment