Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, February 1, 2018

JE NI TIMU ZIPI KATI YA JKT MLALE, KMC NA COASTAL UNION ZITAKAZOKATA TIKETI YA VPL LEO?

KITENDAWILI cha timu zitakazopanda ligi kuu msimu ujao kutoka Kundi B kinatarajiwa kutenguliwa leo kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja tofauti.
Michezo yote ya kundi hili inatarajiwa kuanza saa 10:00 kamili  ioni kukwepa upangaji wa matokeo.
Coastal Union watakuwa ugenini katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro  kucheza na Mawenzi Market, mchezo ambao ni muhimu kwa Coastal yenye pointi 23 kushinda ili wapande daraja.
Vinara JKT Mlale itakuwa nyumbani kuikabili KMC kwenye uwanja wa Majimaji Songea, kwasababu timu hizi zina pointi 25 kila moja inahitaji kushinda ili ipande ila endapo zitatoka sare na Coastal kushinda basi JKT itapanda kutokana na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Coastal ili kujiweka pazuri inatakiwa kushinda kwa idadi ya mabao matatu ili kujihakikishia nafasi moja endapo JKT na KMC watatoka sare JKT na Coastal zitapanda kwa sababu zina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa na KMC italazimika kusubiri msimu ujao.
Michezo mingine katika kundi hili Mufindi itaikaribisha Polisi Tanzania yenye pointi 19 ambayo inashika nafasi ya nne na Mbeya Kwanza itakuwa nyumbani kuikabili Polisi Dar es Salaam ambayo imeshashuka daraja.
 Msimamo wa hili JKT Mlale inaongoza ikiwa na pointi 25 sawa na KMC lakini zikiwa zimetofautiana katika mabao ya kufunga na kufungwa, Coastal Union ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 23, Polisi Tanzania ina pointi 21, Mbeya Kwanza pointi 19, Mufindi United ina pointi 13, Mawenzi Market ina pointi 8 na Polisi Dar es salaam pointi 5.

Michezo ya kundi A inatarajiwa kuchezwa Februari 5 na kundi C itacheza Februari 4.

No comments:

Post a Comment