Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, November 24, 2017

MECHI YA AFCON YA TAIFA STARS DHIDI UGANDA YASOGEZWA MBELE


SHIRIKISHO la Soka barani Afrika (CAF) limesogeza mchezo wa kufuzu mataifa ya Afrika (AFCON) kati ya Tanzania na Uganda kupisha timu za Taifa zilizofuzu fainali ya Kombe la Dunia zitakazofanyika Urusi 2018 kujiandaa.
Mchezo huo awali ulikuwa huchezwe Machi 2018 lakini umesogezwa hadi Septemba 2018.
Taarifa ya CAF inasema mchezo huo ulikuwa huchezwe Machi 18 hadi 26 lakini sasa utachezwa Septemba 3 hadi 11.
Tanzania ipo Kundi  L pamoja na timu za Cape Verde, Uganda na Lesetho.

Kila timu imecheza mchezo mmoja huku Tanzania ikiwa imecheza nyumbani na Lesotho na kutoka sare ya bao 1-1.

No comments:

Post a Comment