Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, November 26, 2017

IBRAHIM CLASS ATETEA MKANDA WAKE


BONDIA, Ibrahim Class amefanikiwa kutetea taji lake GBC uzito wa Lightweight baada ya kumshinda kwa pointi bondia Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini.
Class alishinda kihalali kwani alipigana vizuri na kwa tahadhari kuanzia raundi ya kwanza hadi ya 10  akitumia staili ya Orthodox ambayo ni ya ngumi za kudonoa.
Katika pambano hilo, Class hakuwa na kazi nyepesi ulingoni, kwani alikutana na bondia mwenye ngumi nzito na mzoefu lakini akahimili vishindo vyote na kuwafurahisha watu waliojitokeza Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kumshangilia.
Raundi ya nane Class alimpiga Sibiya ngumi ya pua na kusababisha kuvuja damu na kuanzia raundi alianza kutawala pambano kwani raundi za awali walionekana kupigana sawa.  
Class amefanikiwa kutetea ubingwa huo ambao aliutwaa Julai 1, mwaka huu baada ya kumpiga Jose Forero wa Panama kwa pointi Berlin, Ujerumani.
Akizungumza baada ya mchezo huo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Dk Harrison Mwakyembe alisema amefurahiswa na ushindi aliopata Ibrahim Class na kuahidi kumpa ushirirkiano zaidi ili aendelee kufanya vizuri katika mashindano mengine
“Siri ya mafanikio katika michezo ni kufanya mazoezi, kujiamini kusikiliza mafundisho ya kocha pamoja na nidhamu, Class ni mwanamasumbwi anaepaswa kuigwa na mabondia na wanamichezo wengine wote kutokana na uwezo wake wa kujituma ili wafanikiwe na kuitangaza nchi yetu kimichezo,” alisema Dk. Mwakyembe.
Naye bondia Ibrahim Class ameishukuru serikali kwa ushirikiano iliyompa wakati wa mazoezi mpaka amefanikiwa kupeperusha vyema bendera ya Tanzania na ameahidi kuendelea kufanya vizuri zaidi kila atakapokuwa ulingoni na kushinda mataji na mikanda mingi zaidi.
Class amecheza mapambano 25 na kushinda 21 na amepoteza mapambano manne. 
 

No comments:

Post a Comment