Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, October 15, 2017

Tamasha la Mziki Mnene laacha historia Jijini Mwanza

Binagi Media Group
Maelfu ya wapenzi wa burudani Jijini Mwanza jana wamefurahia tamasha la Mziki Mnene linaloandaliwa na EFM radio na ETV za Jijini Dar es salaa ambapo wasanii mbalimbali akiwemo Kala Jeremiah walipata shangwe kubwa kwenye tamasha hilo lililofanyika uwanja wa CCM Krumba.

Wasanii wengine waliokonga nyoyo za mashabiki zao ni TID, Snura, Young Killer, Baraka Da Prince, Shoro Mwamba pamoja na Msaga Sumu huku Stone Fire akiibuka mkali wa Singeli Michano Mwanza baada ya kuwabwaga washiriki zaidi ya 20.

Afisa Uhusiano wa EFM Radio, Jesca Mwanyika anasema tamasha hilo mbali ya kuwa ni sehemu ya shukurani kwa wasikilizaji wa redio hiyo pamoja na watazamaji wa TVE, pia limelenga kuibua na kuendeleza vipaji vya wasanii hususani wa Singeli.


Tayari limekwisha fanyika katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es salaam, Mtwara na Mwanza na kwamba litaendelea katika mikoa mingine hivyo mashabiki wa burudani waendelee kufuatilia EFM Radio na TVE kwa taarifa mbalimbali ikiwemo tamasha la Mziki Mnene linalopewa nguvu na Biko pamoja na Cocacola.
Mkali wa Singeli, Msaga Sumu akidondosha burudani kwenye jukwaa la Mziki Mnene CCM Kirumba Jijini Mwanza. Shoro Mwamba akishambulia jukwaa la Mziki Mnene na ngoma za moto moto za Singeli. Young Killer alikonga nyoyo za mashabiki zake Jijini Mwanza. Kala Jeremiah alidondosha burudani kali kiasi cha mashabiki kugoma asishuke jukwaani. Mnyama TID akitumbuiza kwenye jukwaa la Mziki Mnene Jijini Mwanza.  Shangwe za wapenzi wa burudani Jijini Mwanza kwenye tamasha la Mziki Mnene. Attachments area Preview YouTube video Tamasha la Mziki Mnene laacha historia Mwanza

No comments:

Post a Comment