TAIFA Stars
jana ilitoka sare ya bao 1-1 na Malawi ‘The Flames’ katika mchezo wa kirafiki
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku Kocha Mkuu, Salum Mayanga akilia na
mwamuzi Israel Nkongo kwamba hakuitendea haki timu yake.
Mayanga
akizungumza baada ya mchezo huo, alisema vijana wake walicheza vizuri, lakini
baadhi ya matukio yaliyokuwa yakiamriwa na Nkongo hayakuwa mazuri kwa Stars na
kwamba hakuchezesha vizuri.
Katika
mchezo huo Stars ilimaliza ikiwa na wacheza pungufu uwanjani, baada ya beki
Erasto Nyoni na kiungo Muzamiru Yassin kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa
nyakati tofauti kipindi cha pili.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na Nkongo aliyesaidiwa na Frank Komba na Soud Lila
wote waaamuzi wenye beji ya Fifa na raia wa Tanzania, mashabiki walishuhudia
Malawi ikienda mapumziko ikiwa na bao 1-0 lililofungwa na Robert Ng’ambi dakika
ya 35 kwa kichwa akitumia vyema makosa ya mabeki wa Stars.
Washambuliaji wa Taifa Stars wakiongozwa na nahodha Mbwana
Samatta na Simon Msuva walipata nafasi kadhaa za kufunga, lakini umaliziaji
haukuwa mzuri. Bao la Stars lilifungwa na Msuva dakika ya 57.
Dakika ya 75 mwamuzi Nkongo alimpandisha jukwaani Kocha Mkuu wa Malawi, Ron van Geneugden kutokana na utovu wa nidhamu, kabla ya Nyoni kuoneshwa kadi nyekundu baada ya kumpiga mchezaji wa Malawi, Mbulu Richard. Kabla ya dakika ya 89 Muzamiru kuoneshwa kadi ya pili ya njano iliyofuatiwa na nyekunu kwa kosa la mchezo mbaya.
Stars: Aishi Manula,
Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Abdi Banda, Kevin Yondan, Himid Mao, Simon
Msuva/Adul Hilal, Hamisi Abdallah/Muzamiru Yassin, Mbwana Samatta, Raphael
Daudi/Mbaraka Yussuf na Shiza Kichuya/Ibrahim Ajibu.
No comments:
Post a Comment