Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata,
Vivian Shalua (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Miss Univerese mwaka
jana, Jihan Dimachk (Kulia) na Miss Earth Tanzania, Lilian Loth.
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limeipongeza kampuni ya Compass
Communications Tanzania kwa kufanya mashindano bora ya Miss Universe hapa
nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Ukuzaji
Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua wakati wa kufanya tathimini ya
mashindano hayo na mashindano ya urembo kwa ujumla.
Mrembo Jihan Dimachk alishinda taji la Miss
Universe mwaka jana huku Lilian Loth akishinda nafasi ya pili katika
mashindano hayo.
Shalua alisema Basata wamefarijika sana na jinsi
mashindano hayo yanavyoendeshwa na hakuna malalamiko yoyote kuhusiana na zawadi
na upendeleo.
Alisema kuwa kutokana na utaratibu mzuri wa
mashindano yao, Basata imeridhia waandaaji wa mashindano hayo, kufanya
mashindano ya mwaka huu na vile vile kuandaa mashindano ya kutimiza miaka 10
tokea kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 2007.
“Pamoja na kuwa na shindano moja kwa
kushirikisha warembo wa mikoa tofauti, bado Basata imefarijika na jinsi
mnavyoendesha na utaratibu unaotumia kuwapata warembo, uendeshaji wa mashindano
mpaka kumpata mshindi,”
“Tunajua kuwa kuna changamoto za wadhamini na
kusababisha kufanya mashindano yenye kalenda fupi na kuondoa mlolongo wa
matukio, hatua hii ni bora zaidi ili kuondoa malalamiko ya zawadi na mambo
mengine, huu ni mfano wa kuigwa,” alisema Shalua.
Mkurugenzi wa Compass Communications ambaye pia
ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai aliishukuru Basata
kwa usimamiaji bora wa mashindano katika sekta ya sanaa nchini na kusema kuwa
watajihidi kuongeza wigo ili kuona warembo wengi zaidi kutoka mikoa tofauti
wanashiriki katika mashindano yao.
Maria alisema kuwa pamoja na changamoto zote wanazokabiliana
nazo, bado wanahitaji msaada kutoka Basata ili kupata wadhamini na kufikia
malengo yao katika kuendeleza Sanaa hapa nchini.
“Kwa sasa kuna changamoto kubwa ya wadhamini wa
mashindano, kuna haja ya kupata msaada kutoka Basata ambao ni chombo cha
serikali, mnaweza kutusaidia kupata wadhamini hata kwa Wizara ya Maliasili na
Utalii, sisi tunatangaza jina la nchi na utalii pia, tunaamini kupitia kwenu,
tunaweza kupata sapoti kubwa kutoka wizara hiyo, Bodi ya Utalii (TTB) na
mamlaka ya zake kama Tanapa,” alisema Maria.
|
Wednesday, October 4, 2017
BASATA YAPONGEZA WAANDAJI WA MISS UNIVERSE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment