KLABU ya Paris St Germain ya nchini Ufaransa imelishtua shirikisho la
soka barani Ulaya (UEFA) baada ya kumsajili kinda Kylian Mbappe kwa dau
kubwa ikiwa ni wiki chache baada ya kuvunja rekodi kwa kumsajili
Neymar kwa gharama ya paundi 198 milioni.
Katika dili la Mbappe, PSG walikuwa na nafasi ya kuchagua aidha
kumchukua kwa mkopo au kumsajili lakini imeonekana ni lazma kwa Monaco
kuwauzia kinda huyo kwa paundi 166 milioni 2018 majira ya joto na
kufanya usajili huo kuwa wa pili katika rekodi za usajili.
Chombo hicho kikubwa cha mpira wa miguu barani Ulaya kilitoa taarifa kuwa
“Kamati ya UEFA ya uchunguzi na Udhibiti wa Fedha za klabu imefungua
uchunguzi rasmi juu ya Paris St Germain kama sehemu ya ufuatiliaji
unaoendelea wa klabu chini ya kanuni ya kifedha ya Financial Fair Play
(FFP)”
Nasser Al-Khelaifi ambaye ni mwenyekiti wa Paris St
Germain alinukuliwa akisema “Kama una wasiwasi kuwa klabu yangu imekiuka
taratibu za usajili wa Neymar inakupasa utulie na kunywa kahawa kwani
hakuna tatizo”
FFP ilianzishwa ili kulinda uchumi wa klabu mbalimbali ziweze kutumia
fedha kutokana na mapato yanayopatikana na kutotumia fedha zitokanazo
na mfuko wa mmiliki wa klabu.
No comments:
Post a Comment