MTANZANIA
Abdulnasir Aziz anayecheza soka kwenye kituo cha Barcelona ya Hispania
anatarajiwa kushuka kwenye dimba la Uhuru Dar es Salaam kucheza mchezo wa
kirafiki wa kimataifa dhidi ya Botswana leo.
Abdulnasir
yupo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na amefanya
mazoezi tangu jana na leo na kocha Mayanga alisema anatarajia kumtumia kwenye
mchezo wa kesho.
“Abdulnasir
anacheza Barcelona kwenye timu ya watoto lakini kwa sasa yupo mapumziko na
nimemwogeza katika kikosi na kesho nitamtumia kwenye mechi kwani amefanya
mazoezi na wenzake,” alisema Mayanga.
Abdulnasir
yupo kwenye program ya Aspire alijiunga Barcelona Februari mwaka huu akitokea
akademi ya Dream Afrika.
Pia Mayanga alisema ameandaa kikosi chake vizuri kwa
kushirikiana na benchi lake la ufundi hivyo anatarajia kuendeleza rekodi ya
kuifunga Botswana.
“Botswana nilicheza
nao na ulikuwa mchezo wangu wa kwanza tangu niteuliwe kuingoza Taifa Stars na
niliwafunga mabao 2-0 na safari hii lazima tuwafunge tena,” alisema Mayanga
aliyeteuliwa Januri 4
Pia Mayanga alisema kufanya vizuri kwa Taifa Stars inasaidia
kuwatangaza wachezaji nje ya nchi na nchi kupanda kwenye viwango vya ubora vya
FIFA ambavyo hutolewa kila mwezi.
Mayanga ameingoza Taifa Stars kwenye michezo 10 tangu aanze
kuwa kocha wa timu hiyo na amefungwa mchezo mmoja, sare minne na kushinda mitano.
Michezo hiyo na Matokeo yake ni dhidi ya Botswana 2-0,
Burundi 2-1, Malawi 2-0, Mauritius 1-1, Angola 0-0, Afrika Kusini 1-0, Zambia
ikashinda 4-2, Lesotho 4-3, Rwanda 1-1 na 0-0.
Naye kocha wa Botswana David Bright alisema kikosi chake
kimechoka na walianza mazoezi jumatatu kwani wachezaji walikuwa kwenye timu zao
lakini hatarajii kupoteza mchezo huu.
Kikosi cha
Taifa Stars ni magolikipa; Aishi Manula, Mwadini Ally na
Ramadhani Kabwili
Mabeki;
Gardiel Michael, Kelvin Yondan, Boniface
Maganga, Abdi Banda, Salim Mbonde na Erasto Nyoni.
Viungo ni Himid Mao Hamisi Abdalla, Muzamiru Yassin, Said Ndemla, Shiza Kichuya, Simon Msuva, Farid Mussa na Abdulnasir Aziz.
Washambuliaji ni Raphael Daud, Kelvin Sabato, Mbwana Samatta na Elius Maguli.
Viungo ni Himid Mao Hamisi Abdalla, Muzamiru Yassin, Said Ndemla, Shiza Kichuya, Simon Msuva, Farid Mussa na Abdulnasir Aziz.
Washambuliaji ni Raphael Daud, Kelvin Sabato, Mbwana Samatta na Elius Maguli.
No comments:
Post a Comment