LIGI Daraja
la Pili Tanzania Bara (SDL), inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 30,
mwaka huu kwa timu kuchuana katika viwanja vitano tofauti.
Akizungumza
na wandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa Shrikisho la Soka Tanzania (TFF)
Alfred Lucas alisema michezo itakayochezwa siku hiyo Kundi A ni kati ya Abajalo
na Cosmopolitan, Namungo na Reha kundi B kutakuwa na mchezo kati ya Pepsi na
Madini.
Kundi C
kutakuwa na mchezo kati ya Burkinafaso na Ihefu, Boma itacheza na Mkamba
Rangers huku Kundi D likikutanisha timu za Bulyanhulu na Mirambo.
Mchezo kati
ya Nyanza FC na Area C uliokuwa ufanyike Septemba 30, 2017 kwenye Uwanja wa
Sheikh Amri Abeid Arusha, sasa utachezwa Oktoba 01, 2017 siku ya Jumapili
kwenye Uwanja huo huo.
Lucas
alisema sababu za mabadiliko haya yanatokana na kuwepo kwa mchezo kati ya Pepsi
FC vs Madini FC ambao utachezwa Septemba 30 katika uwanja huo.
Awali mchezo
wa Nyanza na Area C ulipangwa kufanyika mkoani Manyara, lakini kutokana na hali
ya uwanja ilibidi Bodi ya ligi ufanye mabadiliko husika.
No comments:
Post a Comment