Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, August 5, 2017

YANGA YAACHANA RASMI NA MKATA UMEME

Katibu Mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa amethibitisha kwamba, wameamua kuachana na kiungo wa ulinzi  Justine Zulu ‘mkata umeme’ aliyesajiliwa msimu uliopita wakati wa dirisha dogo la usajili  Disemba, 2016.
Mkwasa amesema Yanga haijaridhishwa na kiwango cha Zulu tofauti na walivyotarajia hivyo wameamua nafasi yake wampe mtu mwingine na yeye waachane nae.
“Zulu alisajiliwa na Yanga mkataba wake ulikuwa mwaka mmoja na bila kuficha wala kupepesa macho performance haikuwa vile ambavyo ilitarajiwa wakati amekuja kusajiliwa kwa hiyo klabu ikaona kwamba, kwa sababu ina malengo ya kutazama mbele zaidi kwa hiyo ikaamua kufanya mabadiliko na kumpa nafasi mtu mwingine.”
“Kwa hiyo tumekaa na agent wake na tumefikia mwafaka, tutafanya taratibu za kumfidia katika kipindi hiki cha siku chache ili tuachane nae kwa moyo mkunjufu kabisa na katika hali ya amani bila kupelekana FIFA.”
Zulu alicheza mechi ya kwanza akiwa na jezi ya Yanga wakati walipokutana na JKU ya Zanzibar kwenye mchezo wa kirafiki, aliingia kipindi cha pili akitokea kwenye benchi.