KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali (TSN) pamoja na Shirika la Utangazaji
nchini (TBC) kesho Ijumaa (Agosti 11, 2017)wameandaa kipindi maalum kwa
wagombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF)
kitakachofanyika mjini Dodoma kuanzia majira ya saa 3 usiku.
Kipindi
hicho maalumu kitarushwa mubashara kupitia TBC pamoja na ‘TSN Online’
kitawakutanisha wagombea urais; Ally Mayay, Fredrick Mwakalebela,
Wallece Karia, Shija Richard, Iman Madega na Emmanuel Kimbe ikiwa ni saa
chache kabla ya siku ya uchaguzi yaani kesho Jumamosi
Mwenyekiti
wa Kamati ya maandalizi ya kipindi hicho, Enock Bwigane alisema kuwa
ili mpira wa miguu uendelee kukua nchini TBC na TSN iliona ni vyema
ikawakutanisha wagombea kwenye jukwaa moja ili waweze kuwaambia wananchi
ni kwa njia gani wataweza kuinua soka la Tanzania kama wakipewa dhamana
hiyo.
Alisema, “Kuna takribani wapiga
kura 130, wagombea urais ni sita lakini mmoja ndiye atakayeshinda na
kuongoza shirikisho hilo kwa miaka minne kabla ya uchaguzi mwingine
hivyo tumeona haja ya kuwakutanisha na kuwawezesha wananchi waweze
kuwafahamu...
“…Naamini fursa ya
kuwakutanisha na kuwapa nafasi ya kuwaeleza watanzania sera na mipango
yao ya kuboresha soka ni jambo la msingi na ni haki yao ukizingatia kuwa
leo ndiyo siku ya mwisho ya kampeni,” alisema Bwigane.
Naye
Katibu wa kamati hiyo, Alfred Lasteck alisema kuwa TSN ikishirikiana na
TBC inatambua nini watanzania wanataka kufahamu kuhusu mpira wa miguu
na ndiyo maana imepanga kuwakutanisha wagombea ili waweze kuzungumza na
umma kabla ya uchaguzi hapo kesho.
“Kuna
zaidi ya Watanzania milioni 50 ambao wangependa kufahamu ni nini
kitasaidia soka la Tanzania ili liweze kuendelea kutoka lilipo sasa hadi
kufikia mafanikio.
“Hivyo ni nafasi ya
kipekee kwa kila mtanzania kufuatilia matangazo mubashara
yatakayorushwa na TBC1 pamoja na TSN Online kipindi kile ambacho
wagombea wote wa Urais watakapokuwa wakielezea mipango yao kuhusu mpira
wa miguu nchini,” alisema Lasteck.
No comments:
Post a Comment