SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemwandikia barua
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB) likimtaka kuwaajibisha maofisa waliyohusika
kupanga ratiba ya Ligi Kuu bila kufuata matukio ya mwaka ya kisoka ya nyumbani
na kimataifa.
Akizungumza
na wandishi wa habari jana, Kaimu Katibu Mkuu alisema ratiba ya ligi ilitakiwa
kukidhi mechi za kimataifa za Taifa Stars kulingana na kalenda ya FIFA, mechi
za mashindano za CAF na FIFA, mashindano ya Mapinduzi, mashindano ya Federation
(Azam Federetion Cup ) na mashindano mengine ambayo yapo kwenye kalenda ya TFF.
“Baada ya ligi kuanza na kusimama Rais Wallace
Karia ameniagiza kumwandikia Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi kumchukulia hatua za
kinidhamu wataalamu wa kupanga ratiba ama kwa uzembe au kwa kutokujua, ”
“Ligi baada
ya kuanza na kuchezwa mzunguko mmoja ililazimika kusimama kupisha mchezo wa
kirafiki wa kimataifa wa Taifa Stars dhidi ya Botswana hali iliyozua maswali
juu ya weledi na utendaji kazi wa TFF,” alisema Kidao
Alisema kati
ya mambo ambayo yamekuwa yakisemwa vibaya ni juu ya ratiba ya ligi kuu kupanguliwa
na kudai yeye kama kocha na mkufunzi anajua athari gani kitaalamu ambazo timu
zinapata achilia mbali kujiandaa kiuchumi.
Alisema Bodi
ya ligi ni chombo cha TFF ambacho wamekipa majukumu ya kusimamia ligi ili TFF
ijikite kwenye maendeleo ya soka kwani
wanaamini wasingeweza kusimamia ligi na wakati huo huo wajikite kwenye
maendeleo.
Pia Kidao
alisema kwa kutambua umuhimu wa kuwa na ratiba ambayo ligi inachezwa mwanzo
mwisho bila kubadilishwa kwa nchi za wenzetu wanavyofanya ameunda kikosi kazi
cha watu wanne ambao kitaipitia ratiba yote na kuipanga na kuiwasilisha
Septemba 2.
“TFF
hairidhishwi na ratiba iliyopo kwani ina mapungufu mengi, hivyo nimeunda kikosi
kazi cha wataalamu wanne kuifanyia kazi na tunaamini baada ya marekebisho hayo
haitabadilika tena mpaka msimu uishe labda litokee kwa jambo ambalo lipo nje ya uwezo mwanadamu
kama mvua,” alisema Kidao.
Kidao
alisema baada ya udhaifu huu kutokea ratiba ya ligi haitatoka bila kusainiwa na
Katibu Mkuu wa TFF ili kulinda heshima ya taasisi hiyo kwani pia ratiba
iliyotoka kuna timu zinamaliza mechi nne ugenini jambo ambalo halina ushindani
sawa.
Mtandao huu ulimtafuta Mtendaji wa Bodi ya Ligi, (TPLB) Boniface Wambura kujua ni hatua
gani alizochukua juu ya watendaji wa bodi hiyo ambao wanalalamikiwa na kudai
hajapata barua kutoka TFF akipata ataeleza hatua alizochukua.
Pia nilitaka
kujua kama anaridhika na ratiba iliyotoka bila kuzingatia kalenda ya FIFA na
kusema upangaji wa ratiba siyo kazi ya professionalism.
Baada ya
ligi kuu kuanzia Agosti 26 kuanza ligi ilisimama baada ya kuchezwa mzunguko
mmoja hali iliyozua maswali huku tuhuma zingine zikitupwa kwa uongozi mpya wa
TFF ambao uliingia madaraka mapema Agosti.
Kwa miaka
kadhaa TPLB ambayo ndiyo waandaji wa ratiba za ligi zote imekuwa ikilalamikiwa
kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara na kugeuka kero miongoni mwa wadau wa
soka nchini.
No comments:
Post a Comment