MCHEZAJI wa
kimataifa wa Tanzania anaeichezea klabu ya Difaa El Jadid ya Morocco, Simon
Msuva amesema anapata tabu kwenye lugha
kwani nchi hiyo wanazungumza sana Kiarabu na Kifaransa kidogo.
Msuva ambaye
alitua nchini jana usiku kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya
Botswana unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam
alisema Morocco ni nchi ya kiarabu na yeye hajui Kifaransa wala Kiarabu lakini
kwa sababu lugha ya mpira ni moja uwanjani wanaelewana.
“Lugha za
mazungumzo nitajifunza taratibu kwa sababu nina miaka mitatu pale. Yupo ‘psychologist’
ambaye anajua Kiingereza kidogo na ameniahidi kunitafutia mwalimu wa
kunifundisha kiarabu na Kifaransa,” alisema Msuva.
Pia Msuva
alisema kocha wake wa Jadid amembadilishwa nafasi ya kucheza kutoka namba 9
uwanjani lakini hakujamwathiri chochote kwani kama mchezaji kocha anaweza kuona
unafaa kucheza nafasi gani kulingana na mfumo wake.
“Hapa
nilikuwa nacheza kama kiungo mshambuliaji nikitokea pembeni kushoto au kulia ni
kocha tu anaamua anitumiaje kulingana na mfumo wake. Kocha wangu wa Jadid
ameona nafaa kwenye umaliziaji na niko vizuri kwenye ‘movement’ aliniambia
aliniona mara kadhaa na akasema anahitaji kuona uwanjani kile alichokuwa
akikiona kwenye picha mjongeo ‘video’,” alisema Msuva.
Msuva
alisema katika mechi alizocheza ameonesha uwezo wake hadi sasa anacheza kama
namba 10 lakini pia anacheza nafasi yoyote ya mbele kwa sababu anahitaji
kufunga na pia anahitaji kutengeneza nafasi tangu akiwa mdogo alikuwa anacheza
namba 9 au 10.
Msuva
alisema kuna vyakula amekutana navyo kule huku alikuwa anaringa kula lakini
kule inabidi ale na wao wanasisitiza kula kwa sababu wanasema vinamjenga
mchezaji endapo utazingatia kula kwa wakati na kusema anakosa ugali wa dona
Aidha Msuva
alisema alipofika alipokelewa vizuri na ameweza kufanya kitu ambacho wao
wenyewe wameona anafaa kuwa pale kwa hivyo hakuna tofauti sana na Tanzania.
Msuva
alisema malengo yangu ni kusogea zaidi kwa sababu ligi ina ushindani ila hadi
sasa amecheza mechi 11 na amefanikiwa kufunga mabao tisa
No comments:
Post a Comment