SHIRIKISHO
la Soka Barani Afrika (CAF) limesitisha kozi zote za makocha kwa nchi wanachama
hadi mtaala mpya utakapotoka.
Akizungumza
na wandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) Salum Madadi alisema CAF
imesimamisha kozi za leseni C, B na A kwa ajili ya kuweka/kuandaa mtaala mpya.
“Tunaomba
wale wote ambao walikuwa wamejiandikisha na kulipa ada kwa ajili ya kozi
mojawapo wawe wavumilivu mpaka hapo tutakapopata maelekezo toka CAF,” alisema
Madadi
Pia Madadi
alitumia fursa hiyo kuomba radhi kwa hatua hiyo ya Caf.
Aidha kamati
ya Ufundi ya TFF inatarajiwa kukutana Septemba 24 kuona namna ya kuendesha kozi
hizo kwa wale ambao walikuwa tayari wameshalipa.
No comments:
Post a Comment