MSHAMBULIAJI
wa Kimataifa wa Simba, Emanuel Okwi leo ameisaidia timu yake ya Taifa, “Uganda
the Crane’ kuifunga Misri bao 1-0 kwenye mchezo kufuzu fainali za Dunia
zitakazofanyika Russia 2018.
Uganda
ambayo ilikuwa ikicheza nyumbani kwenye Uwanja wa Taifa wa Mandela ilipata bao
dakika ya 51 likifungwa na Emanuel Okwi kwa shuti baada ya kuichambua ngome ya
Misri kutoka upande wa kulia.
Akizungumza
baada ya mchezo huo, Okwi alisema wamefurahi kushinda mchezo huo lakini
wanajiandaa kwa mchezo wa marudiano ambao unatarijiwa kuchezwa Alexanderia
Misri Septemba 5.
Kocha wa
Uganda The Cranes, Moses Basena alisema nilipowaita wachezaji niliwaambia juu
ya mchezo huu na ushindi tu lakini kocha wa Misri Hector Cuper alisema uwanja
ulikuwa mbaya na walijaribu namna nyingi lakini hawakufanikiwa
“Tuna
michezo ya kushinda na tuna pointi 6 hivyo tunaamini tutashinda nyumbani,”
alisema Cuper.
Kutokana na
mchezo huo wa marudiano Simba itawakosa Okwi na Juuko kwenye mchezo dhidi ya
Azam FC unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Septemba 6.
Kikosi cha Uganda
ni Dennis Onyango, Nico Wakiro Wadada, Godfrey ‘Jajja Walu’ Walusimbi, Isaac
Isinde, Murushid Jjuuko, Khalid Aucho, Emmanuel Arnold Okwi, Hassan Wasswa
Mawanda, Faruku Miya, Derrick Nsibambi, Joseph Benson Ochaya
Kikosi cha
Misri ni Essam El Hadry, Fathy, Hegazi, Ramy Rabea, Shafy, Tarek Harmed,
Muhammed ElNeny, Hassan ‘Trezegeut’ Mohamoud, Abdalla, Muhamed Salah, Kahraba
No comments:
Post a Comment