WACHEZAJI
Obrey Chirwa wa Yanga na Deus Kaseke wa Singida United wameachiwa huru na
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la mpira miguu Tanzania (TFF) baada ya
kufungiwa kutocheza michezo ya kimashindano ya ndani ya nchi kwa tuhuma za
kufanya vurugu katika mchezo wa mwisho ya Ligi Kuu msimu uliopita dhidi ya Mbao
FC.
Katika
mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mei 21 mwaka huu wachezaji
hao ambao walikuwa wakichezea Yanga ilidaiwa kumwangusha mwamuzi wa mchezo huo
Charles Ludovic kutoka Tabora kutokana na kutoridhishwa na maamuzi.
Akizungumza leo Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya nidhamu ya TFF, Peter Hellar alisema wamepitia
picha mjongeo (video) mnato, taarifa ya mwamuzi na Kamishna na kujiridhisha
kuwa wachezaji hao hawakufanya kosa bali Simon Msuva ndiye aliyemsukuma Ludovic
na kuandikiwa barua ya onyo.
“Kamati ya
nidhamu ya TFF imekutana jana (juzi) kusikiliza shauri la wachezaji Deus
Kaseke, Obrey Chirwa na Simon Msuva. Chirwa na Kaseke walikuwepo na kuhojiwa lakini
Msuva hakuwepo,”
“Kupitia picha
mjongeo (video) kamati imejiridhisha kuwa Chirwa na Kaseke hawakufanya kosa ila
Msuva licha ya kutokufika mbele ya kamati amepatikana na hatia na ameandikiwa
barua ya onyo,” alisema Hellar.
Pia Hellar
alisema kwa mujibu wa kanuni za ibara ya 49 kifungu kidogo cha tisa ambayo
adhabu yake ni kufungiwa si chini ya mechi tatu imeamua kutoa onyo kwa sababu
kamati ya saa 72 ilitoa adhabu kabla ya kamati ya nidhamu ambayo ndio yenye
mamlaka ya kutoa adhabu.
Aidha Hellar
alisema kwa kutambua kuwa wachezaji hao walianza kutumikia adhabu kabla ya
kamati ya nidhamu kusikiliza shauri hilo na Yanga ilikuwa kwenye mashindano
imeamua kumwandikia Msuva barua ya onyo
Tayari Kaseke
na Chirwa wamekosa mchezo wa kwanza wa ligi huku Msuva akisajiliwa na timu ya
Difaa Al Jadida ambayo inashiriki ligi kuu ya Morocco.
Shauri hilo
liliwasilishwa kwa kamati hiyo mnamo Mei 30 na Kamati ya uendashaji wa Ligi kwa
hatua za kinidhamu.
No comments:
Post a Comment