RAIS wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA), Gianni Infantino na chama cha soka Rwanda, wametuma salamu za pongezi
kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) Wallace Karia kwa
kuchaguliwa kuwa Rais kwa kipindi cha miaka minne ijayo ya 2017-2021.
Akizungumza na wandishi wa habari, Ofisa
Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema, Infantino katika barua yake ya Agosti 14,
2017 alimpongezi Karia na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake na kusema
hana shaka na uwezo wake.
“Kwa wakati wote, nakuhakikishia ushirikiano
wa kutosha kutoka FIFA katika malengo yako na milango iko wazi wakati wote wewe
kuja kujadili masuala ya mchezo wa mpira wa miguu hasa eneo la utawala.
“Nimeagiza upande wa utawala kuwasiliana nawe
kuona na kupanga tarehe rasmi ya safari, nikutakie kheri na fanaka, nguvu na
kila aina ya mafanikio katika majukumu yako mapya huku nikitarajia ujio wa
kuonana nawe haraka,” alisema
Pia barua hiyo inasema Infantino hana hana
shaka na uwezo wa Karia ukizingatia alikuwa Makamu wa Rais wa kipindi
kilichopita, hivyo atakuwa fursa ya kuiletea nchi maendeleo ya mchezo soka.
Wakati huo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu
la Rwanda (FERWAFA) nalo kwa upande wake wamempongeza Rais wa TFF, Wallace
Karia kwa kuchaguliwa kuwa kiongozi mpya wa shirikisho.
Wakati huo huo Rais wa shirikisho la Rwanda, (FERWAFA)
Nzamwita Vincent imesema Rwanda itaendelea kuwa bega kwa bega na Tanzania
katika maendeleo ya mpira wa miguu kwa ushirikiano baina ya nchi mbili za ukanda
wa Afrika Mashariki unaounda Baraza la Soka la nchi za Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment