HUKUMU ya
Obrey Chirwa, Simon Msuva na Deus Kaseke inatarajiwa kutolewa kesho baada ya
kamati ya nidhamu kukaa na kusikiliza na kuamua.
Wachezaji
hao wanatuhumiwa kumvamia mwamuzi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC
uliochezwa Mei 20 mwaka huu hukumu yao inatarajiwa kutolewa na kamati ya
nidhamu ambayo mwenyekiti wake ni Abbas Tarimba.
Akizungumza
na wandishi wa habari jana. Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
Alfred Lucas alisema watuhumiwa wote wamejulishwa kufika kwenye shauri hilo.
“Wachezaji
wote wana taarifa na wanatakiwa kufika kwenye kamati kujitetea au kujibu tuhuma
zinazowakabili na nashukuru Msuva naye atakuwepo kwani anatarajiwa kuwasili leo
usiku (jana usiku) alisema Lucas.
Aidha Lucas
alisema shauri hilo lilichelewa kusikilizwa kwani baada ya ligi kumaliza
uongozi wa TFF ulikuwa katika harakati za uchaguzi mkuu uliofanyika mapema
mwezi huu sasa kamati zimepatikana na zimeanza kazi
Kamati ya
saa 72 iliwasimamisha wachezaji hao kutoshiriki mchezo wowote unaosimamiwa na
TFF hadi tuhuma zinazowakabili.
No comments:
Post a Comment