Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 12, 2017

SIMBA NA YANGA KUKUTANA AGOSTI 23 NGAO YA JAMII



WATANI wa jadi Simba na Yanga watakutana Agosti 23 katika mchezo wa ngao ya hisani ikiashiria ufunguzi msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom 2017/18.
Pazia rasmi la ligi hiyo litafunguliwa Agosti 26 ambapo mechi saba zitachezwa katika viwanja mbalimbali nchini ambapo itamalizika Mei 20 mwakani kwa kupatikana bingwa mpya.
Ofisa Habari wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) amewaambia Waandishi wa Habari kuwa mchezo huo wenye kuvuta hisia za mashabiki wengi ndani na nje ya nchi utafanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
"Mchezo wa ngao ya hisani kati ya Simba na Yanga utafanyika Agosti 23 kwenye uwanja wa Taifa ukiashiria kuanza kwa msimu mpya wa ligi 2017/18 na wiki moja mbele itaanza rasmi," alisema Lucas.
Aidha Lucas amesema miamba hiyo itakutana tena Oktoba 14 katika mchezo wa kwanza wa msimu kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa.
Ratiba ya michezo katika wiki ya kwanza ya ligi hiyo.
 
Ratiba ya ligi kuu Agosti 26

Ndanda vs Azam FC
Mwadui FC vs Singida United
Mtibwa Sugar vs Stand United
Simba vs Ruvu Shooting
Kagera vs Mbao FC
Njombe Mji vs Prisons
Mbeya City vs Majimaji



No comments:

Post a Comment