Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, July 22, 2017

LIVERPOOL YAMSAINI BEKI WA HULL ANDREW ROBERTSON

 

Liverpool imemsaini Beki wa Hull City Andrew Robertson kwa Ada ya Awali ya Pauni Milioni 8 ambayo inaweza kuongezeka hadi Pauni Milioni 10.
Robertson, mwenye Miaka 23 na ambae pia huichezea Timu ya Taifa ya Scotland, alijiunga na Hull City kutoka Dundee United ya Scotland kwa Dau la Pauni Milioni 2.85 Mwaka 2014 na kuichezea Mechi 39 Msimu uliopita wakati Hull wakiporomoka kutoka EPL, LIGI KUU ENGLAND, na kutupwa Daraja la chini la Championship.
Uhamisho huu wa Robertson kwenda Liverpool pia utauinufaisha Dundee ambao wanatarajiwa kupata Mgao wa Pauni 600,000.

Robertson anakuwa Mchezaji wa 3 kusainiwa na Liverpool katika kipindi hiki cha Uhamisho na wengine ni Winga wa Egypt alietoka Klabu ya Italy AS Roma Mohamed Salah na Straika Chipukizi kutoka Chelsea Dominic Solanke.