KOCHA Mkuu
wa timu soka yaTaifa, Taifa Stars, Salum Mayanga amejigamba kuifunga Lesotho
leo katika mechi ya kutafuta kufuzu fainali za michuano ya Kombe la Mataifa ya
Afrika (Afcon) 2019 utakaochezwa saa 2 usiku Uwanja wa Azam, Chamazi, Dar es
Salaam.
Akizungumza
na wandishi wa habari jana, Mayanga alisema wamefanya maandalizi ya kutosha kwa
ajili ya mchezo huo kwani miezi miwili iliyopita walicheza michezo miwili ya
kirafiki pamoja na kambi ya ndani na nje waliyokaa.
“Tunacheza
na timu nzuri ambayo msimu uliopita ilionesha kiwango kizuri katika mashindano
haya pia nimeangalia mechi ambazo wamecheza nyuma na kugundua udhaifu wao upo
wapi,” alisema Mayanga.
Pia Mayanga
alisema watacheza kwa kujituma, ufundi na mbinu ambazo wamezifanyia kazi vizuri
hivyo ana uhakika wa kutoka na ushindi.
Naye nahodha
wa timu hiyo, Mbwana Samatta alisema timu ipo vizuri na wachezaji wamejiandaa
vizuri kwa mchezo wa leo.
Kwa upande
wa Kocha wa Lesotho Moses Malieho alisema wamejiandaa vizuri kwa sababu
wanafahamu Tanzania siyo timu rahisi kwani amefuatilia michezo yao ya nyuma
waliocheza na Nigeria na Botswana.
“Tumejiandaa
kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Msumbiji na kushinda 1-0 lakini
tumekuja kupambana kwani Tanzania siyo timu ya kubeza,” alisema Malieho.
Pia alisema
wanajua Tanzania siyo timu ya kubeza kwani ina wachezaji wanaocheza soka Ulaya
na kipindi cha karibuni imekuwa ikifanya vizuri.
Kwa mujibu
wa daktari wa viungo wa Taifa Stars, Gilbert Kigadya alisema wachezaji wote wako vizuri kasoro Mohammed Hussein
'Tshabalala' aliyeumia kwenye mechi ya kombe la FA wa Simba dhidi ya Mbao FC uliochezwa
katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma hivyo hatacheza.
Mechi hii
itachezeshwa na waamuzi kutoka Djibout ambao ni Abdillah Mohammed akisaidiwa na
Gamaladen Abdi na Farham Salime na mwamuzi
wa mezani ni Twagirumukiza Abdulkarim kutoka Rwanda.
Viingilio
vya mchezo ni sh. 5000 viti vya kawaida na sh.10,000 VIP.
Tanzania
ipo kundi L pamoja na timu za Lesotho, Uganda na Cape Verde na kila timu moja
kwenye kila kundi itafuzu katika fainali hizo ambazo zitafanyika 2019 nchini
Cameroon.
Mara
ya mwisho Tanzania kushiriki fainali hizo ni 1980 nchini Nigeria wakati
zikiitwa fainali za Mataifa Huru ya
Afrika lakini kwa miaka ya karibuni imekuwa ikiondolewa katika hatua za makundi.
No comments:
Post a Comment