Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, June 10, 2017

Nairobi Kuhamia Dar, Mashabiki Elfu10 kutua kushuhudia fainali ya SportPesaNairobi kuhamia Dar es salaam kesho pale miamba ya soka nchini Kenya wenye upinzani mkali wa jadi kati ya Gor Mahia na AFC Leopards zitapokutana katika uwanja wa Uhuru katika fainali ya SportPesa Super Cup.
Si mara ya kwanza kwa miamba hii ya soka nchini Kenya kukuta wawili katika ardhi ya ugenini.
Mwaka 1980 katika michuano ya CECAFA ( sasa Kagame Cup ) nchini Malawi walikutana katika fainali baada ya Gor Mahia kuwapiga 4-2 wenyeji Limbe kwenye mikwaju ya penati. AFC Leopards ambao wakati huo walikuwa wakijulikana kwa jina la Abaluhya FC waliitandika timu ya jeshi la Zambia Green Buffaloes 1-0.
Katika fainali hiyo Gor Mahia walishinda 3-2 dakika za jioni kabisa baada ya matokeo ya sare ya 2-2 kudumu mpaka dakika ya 85 .
Ni moja ya fainali za kukumbukwa sana za wababe hawa wa soka nchini Kenya walipokutana nje ya Kenya kwa mara ya kwanza na Gor Mahia kunyakua kombe la CECAFA kwa mara ya kwanza.
SportPesa wanastahili pongezi za dhati kuyaleta mashindano haya Tanzania na kuwapa burudani ya aina yake wadau wa soka Afrika mashariki .
Tayari taarifa za awali zimetanabaisha mashabiki takribani 10,000 toka Kenya wanaingia kesho jijini Dar es salaam kuushuhudia mtanange huu wa kihistori.
Upinzani wa jadi kati ya Gor Mahia na AFC Leopards unajulikana kama ‘ mashemeji ‘ Derby ikiwa mechi namba nne kwa mvuto zaidi Afrika . Ya kwanza ni Al Ahly vs Zamaleki , Kaiser Chiefs vs Orlando Pirates na ya tatu ni Yanga SC vs Simba SC .