Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, June 11, 2017

DAKIKA 90 ZATOSHA KUIUA AFC LEOPARD, GOR MAHIA MABINGWA WA SPORTPESA
INGAWA Gor Mahia na AFC Leopards zinatoka Kenya, lakini kwa matokeo ya leo ya fainali ya SportPesa, wimbo wa msanii wa Singeli Man Fongo hainaga ushemeji tunakulaga, unawahusu.
Hiyo ni kutokana na mechi ya mahasimu hao kujulikana kama mechi ya mashemeji kutokana na uhusiano wa timu hizo kutoka nchi jirani ambapo jana, Gor Mahia ilidhihirisha haina cha ushemeji nyumbani wala ugenini baada ya kuifunga Leopards mabao 3-0.
Matokeo hayo yamedhihirisha umwamba kwa Gor kwani ilipata ushindi kama huo dhidi ya Leopards katika mechi ya Ligi Kuu Kenya mwezi uliopita.
Katika mechi ya jana, iliichukua mpaka dakika ya 60 kwa Gor kuandika bao la kuongoza kupitia kwa Timoyh Otieno aliyefunga bao hilo kwa shuti kali lililomshinda kipa wa Leopards Ian Otieno.
Dakika ya 72 Oliver Maloba aliongeza bao la pili kwa Gor baada ya kupokea pasi nzuri ya George Odhiambo na kuujaza mpira wavuni.
Bao la tatu la mabingwa hao lilifungwa na John Ndorangu katika dakika ya 90 kwa shuti kali akiunganisha pasi ya Odhiambo.
Ushindi huo unaifanya Gor Mahia kupata kitita cha dola za Marekani 30,000 (zaidi ya sh milioni 60) na Leopards ikivuna dola 10,000 (zaidi sh milioni 20).
Timu nyingine zilizoshiriki michuano hiyo ni Simba, Yanga, Singida United, Jangombe Boys na Nakuru All Stars ambazo ziliishia njiani.