Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, June 20, 2017

MARUFUKU KUSAJILI SHULE MPYA BILA KUWA NA VIWANJA VYA MICHEZO




Serikali imesema ni marufuku kwa shule ambayo itakuwa haina viwanja vya michezo kupatiwa kibali cha kufungua shule ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Elimu namba 25 ya mwaka 1978.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Masindano ya kwashule za msingi nchini UMITASHUMTA mkoani Mwanza, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMO) Mh. George Simbachawene, amemuagiza Kamishna wa Elimu nchini, kutozipatia vibali shule zinazo hitaji kufunguliwa endapo zitakuwa hazina viwanja vya michezo.
Simbachawene, amesema kutokana na sheria ya Elimu namba 25 ya mwaka 1978, ambayo inataka kila shule inapofunguliwa lazima iwe na viwanja visivyo pungua vitano hivyo nilazima hili lizingatiwe, “nichukue nafasi hii kumuagiza kamishna wa Elimu kuanzia sasa asisajili shule yeyote ile ambayo itakuwa haina Viwanja vya michezo, kwani bila kufanya hivyo azma yetu yakuinua michezo nchini haiwezi kutimia.”
Mbali na kutoa maagizo hayo waziri Simbachawene, ameziagiza pia halmashauri na wilaya kote nchini kutenga sehemu ya mapato yao ya  ndani kwaajili ya kitengo cha michezo, huku akizihimiza kuweka katika bajeti ijayo ya serikali fedha kwenye vifungu vinavyo husiana na michezo na kuonya kuwa endapo Halmashauri itashindwa kufanya hivyo basi yeye kama waziri mwenye dhamana hatakubali ipite.
Amesema Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 sehemu ya (61) inatambua suala la Michezo lakini pia Sera ya Elimu ya Mwaka 1995, hivyo kama Serikali lazima waweke kipaumbele katika suala zima la michezo.
Ameongeza kuwa, Msingi wa Michezo nchini ni michezo ya UMITASHUMTA NA UMISETA ndio Dira ya timu zetu za Taifa, “Tukiwaandaa vijana wetu vizuri na kutokana kaulimbiu hii ya masula ya viwanda, hatuna wasiwasi kuwa hawa ndio viwanda vyenyewe, mchezaji mmoja aliyefikia viwango vya kimataifa huweza kugharamia hata bajeti ya nchi” alisema Simbachawene.
Katika hatua nyingine Simbachawene, amewaagiza makatibu Tawala kote nchini, kusimamia suala la taaluma na michezo, amesema hakuna taaluma bila Michezo na Hakuna michezo bila Taaluma kwa mantiki hiyo lazima nidhamu ya hali ya juu iongezwe miongoni mwa vijana na wanamichezo kwa ujumla. 

No comments:

Post a Comment