Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, May 30, 2017

TFF YATEUA MAKOCHA 26 WA KUSAKA VIPAJI SHULENI KILA MKOA



SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeteua makocha 26 kwa ajili ya kufanya skauti  za vijana wenye vipaji vya soka kwenye mashindano ya shule za msingi (Umitashumta) na Sekondari (Umisseta) ngazi za mikoa watakaojumuishwa kwa  maandalizi ya michuano ya Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi alisema TFF kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imedhamiria kuboresha mashindano hayo ili kupata vijana wengi wenye vipaji  kuanzia ngazi ya mkoa na Taifa.
Mashindano ya Umisseta ngazi ya taifa yanatarajiwa kufanyika Juni 6 hadi 17 na Umitashumta Juni 27 hadi 28 jijini Mwanza ambapo mikoa itapeleka timu zao kuwakilisha kitaifa.
 “Tumejipanga kwenda kuchagua vijana ngazi ya mkoa na baadaye kitaifa. Tunategemea makocha tuliowateua watatufanyia kazi hiyo kutoka kila mkoa na baadaye kutakuwa na jopo la makocha sita watakaokuwa Mwanza kwenye fainali Umitashumta na Umisseta,”alisema.
Alisema wanataka kuibua vipaji kwa vijana wenye umri chini ya miaka 13 ambao watashiriki  fainali za mataifa ya Afrika chini ya umri wa miaka 17, mwaka 2021. Hivyo maandalizi yaanza kuanzia sasa.
Pia, alisema wataboresha kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 15 watakaoshiriki fainali za vijana chini ya umri wa miaka 17, mwaka 2019. Lakini pia, watachaguliwa vijana chini ya umri wa miaka 20 kuboresha kikosi hicho cha Ngorongoro Heroes.
Makocha walioteuliwa mikoa mbalimbali ni Oscar Mirambo (DSM), Kessy Mziray (Mwanza), Shaweji Nawanda (Mtwara), Charles Mayaya (Shinyanga), Mohamed Muya (Dodoma), Mohamed Laizer (Arusha), Madenge Omari (Mara),Samwel Moja (Lindi), Issa Mgaza (Kilimanjaro), Khamis Mambo (Kigoma), John Nzongwe (Geita), Zakaria Mwamba (Rukwa), Godfrey Mvula (Ruvuma) na Aloyce Mayombo (Pwani),
Wengine ni Osuri Kosori (Simiyu), Gabriel Gunda (Singida) Zahoro Ramadhan (Tanga), Athuman Kairo (Morogoro), Fidelis Kalinga (Iringa), Ally Kagire (Kagera), Mohamed Bachoro (Katavi), Albeti Gama (Njombe), Andrew Nzoma (Tabora), Anthony Mwamlima (Songwe), Gaul Msalia (Mbeya) na Victor Kijazi (Manyara).

No comments:

Post a Comment