TIMU ya
Taifa ya Vijana ya Tanzania, ‘Serengeti boys’ kesho inashuka uwanjani kucheza na Niger
katika fainali za 12 za Afrika kwa vijana Uwanja wa Port
Gentil, Gabon.
Awali
Serengeti boys ilikuwa inacheza kwenye Uwanja wa Stade l’Amitie lakini
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limelazimika kuupeleka mchezo huo katika
Uwanja wa Port Gentil, Gabon ili ichezwe kwa pamoja kutokana na ushindani
uliopo kundi B
Mchezo huo
ambao utaanza saa 12:30 saa za Gabon sawa na 2:30 usiku Tanzania utachezeshwa
na mwamuzi Daniel Nii Ayi Laryea raia wa Ghana akisaidiwa na Seydou Tiama wa
Burkina Faso na Mamady Tere wa Guinea.
Akizungumza
kwa njia ya simu, Kocha Mkuu wa Serengeti boys, Bakari Shime maarufu kama
Mchawi Mweusi, alisema mchezo huo ni muhimu kushinda ili kufuzu kucheza kombe
la dunia.
“Tunamshukuru
Mungu na Watanzania kwa sapoti yao ila naomba waendelee kutuombea kwani mchezo
wa kesho (leo) ni muhimu kushinda ili kufuzu kucheza kombe la dunia,”
“Kauli mbiu
yetu ni Gabon hadi kombe la Dunia na sisi Gabon tumefika sasa tunataka tufike
India kwenye kombe la dunia,” alisema Shime
Pia Shime
alisema baada ya kufanya vizuri michezo ya awali wachezaji wamepata ujasiri na
mchezo na Niger wanaingia uwanjani wakiwa na lengo la ushindi tu.
Mchezo huu wa utatangazwa na radio
Tanzania (TBC), radio one pia utaoneshwa Supersport nine na ZBC1.
Baada ya hatua ya makundi
kumalizika timu mbili zitakuwa zimefuzu hatua ya nusu fainali na kukata tiketi
ya kucheza fainali ya kombe la dunia kwa vijana waliochini ya miaka 17 zitakazofanyika
nchini India baadae Oktoba.
Serengeti
boys inahitaji sare tu kujihakikishia kufuzu nusu fainali na pia kufuzu Kombe
la Dunia baada ya sare ya 0-0 na mabingwa watetezi, Mali na ushindi wa 2-1
dhidi ya Angola ambazo nazo zitacheza muda huo huo Uwanja wa Stade l’Amitie mjini Libreville.
Serengeti
boys ipo kundi B na timu za Mali, Niger na Angola na kundi A lina timu za
Cameroon, wenyeji Gabon, Guinea na Ghana.
No comments:
Post a Comment